Y Tony azidi kupagawa na Kajala

            Msanii wa Bongo Fleva, Y Tony ameendelea kuweka hisia zake wazi kwa mrembo kutoka Bongo Movie, Kajala huku akikanusha tetesi za kuwa na mtoto. Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake ‘Safina’, amesema uwepo wa Kajala ni moja ya sababu za kumfanya yeye kuendelea kujitahidi kufanya muziki mzuri.

 

Kajala anani-inspire sana na ninamuombea kwa Mwenyenzi Mungu azidi kuwepo ilimradi nizidi kufanya vitu vizuri, kwa sababu nampenda sana, yaani katika wasanii wote wa kike ndiye msanii nampenda kutoka kwenye moyo, siongopi na ipo hivyo na pia nashaongea sana na watu wameshasikia,” Y Tony ameiambia E-Newz ya EATV.

 

Alipoulizwa kuhusu mtoto alisema, “mtoto wa nini, mimi sina mtoto, nikipata mtoto utajua ila sasa hivi sina mtoto, labda Mungu akinijalia kwa sababu sasa hivi bado ni kijana mdogo,” alisistiza Y Tony.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*