STAA ELIZABETH MICHAEL ‘LULU’ ANAVYOGEUKA ALMASI YA MITINDO

              Linapokuja swala la mitindo hasa mavazi na mapambo huwezi kuacha kumtaja Elizabeth Michael maarufu kama Lulu, kwenye upande wa mastaa Bongo wanaokimbiza kwa kupendeza.Lulu anafahamika hasa katika uigizaji ila leo tutamtazama katika upande wa mitindo hususani mavazi yake.

 

       Naamini kwa sasa wabunifu wengi wamavazi Afrika Mashariki, wanatamani wamveshe ili waweze kuuza brand za mavazi yao, hii inaweza kuwa fursa pia kwa mrembo huyo. Lulu amekuwa Almasi ya mitindo kwani amewapa sababu wasichana wengi hususani wenye rika lake kujifunza kutoka kwake.

 

        huyo amekuwa akiwapa maswali mbalimbali kwanini anapendeza na anajua kujipatia hii inatokana na kuwa ameutambua mwili wake unatakiwa uvae nini na kwa wakati gani, pia amekuwa akizingatia swala zima la rangi inayoendana na shughuli, vile vile amekuwa akijua aina gani ya make up anatakiwa kupaka ili avutie zaidi.

 

Wengi wetu tumekuwa tukitamani muonekano wa binti huyo ila tumesahau kuwa huwezi kufanya vyote hivyo kama haujiamini na kutunza mwili wako pia na kuijua fashion kwa upana zaidi, ukitazama picha za Lulu unaweza kujifunza kitu.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*