OFM KAZINI… DAKTARI ‘MUUAJI’ ANASWA!

   Mbena akiwa chini ya ulinzi. Jamaa aliyejitambulisha kuwa ni daktari wa hospitali moja iliyopo maeneo ya Buza jijini Dar, aliyetajwa kwa jina moja la Mbena, amenaswa na polisi kwa kushirikiana na kikosi kazi cha kufichua maovu cha OFM cha Global Publishers, akitoa huduma za kimatibabu kinyume na taratibu hivyo kuhatarisha uhai wa wagonjwa. Mbena baada ya kudakwa, akionyesha nayaraka

 

                UCHUNGUZI Kabla ya zoezi la kumtia nguvuni jamaa huyo, uchunguzi uliofanywa ulionesha kuwa, nje ya ‘hospitali bubu’ yake hiyo, ameweka bango la duka la dawa maeneo ya Vingunguti, Kwa-Kombo jijini Dar. Vifaa vyake vya kazi. Baada ya kuvamia kwenye hospitali hiyo bubu, polisi na OFM walishuhudia huduma zinazotolewa za kimatibabu zilizokuwa kinyume na utaratibu ambapo mbali na kuuza dawa, jamaa huyo alikuwa akifanya upimaji wa vipimo mbalimbaali vya malaria, choo, mkojo, UTI na magonjwa mengine makubwamakubwa. Mwenyekiti wa mtaa.

 

                 MASHUHUDA Kwa mujibu wa mashuhuda, jamaa huyo amekuwa akitoa huduma za kimatibabu zinazostahili kutolewa kwenye vituo vikubwa vya afya na hospitalini huku akiwa hana leseni wala kibali chochote kile cha kutoa huduma hizo mahali hapo. Mmoja wa watu walitoa ushuhuda wa shughuli zinazofanywa na jamaa huyo mahali hapo alisema kuwa, mwanaye alizidiwa, akampeleka mahali hapo, lakini cha ajabu usiku alizidiwa tena na alipomkimbiza katika Hospitali ya Amana aliambiwa kuwa dawa alizopewa na daktari huyo hazikuwa za ugonjwa uliokuwa ukimsumbua mwanaye, jambo lililotafsiriwa kuwa ni la hatari na slichokifanya mtu huyo ni ‘uuaji’.

 

                        Niliumia sana baada ya kuambiwa kuwa mwanangu anasumbuliwa na UTI pamoja na minyoo ya Amoeba, lakini akapewa vidonge vya pumu vilivyozidi nguvu mtoto na kama siyo kumuwahisha Amana, leo tungekuwa tunazungumza mengine,” alisema mzazi huyo kwa masikitiko na kuongeza ‘AMBIPU’ KIGWANGALLAH “Kwanza tuna shaka na ujuzi wake. Hatuna uhakika kama ni daktari kweli maana nusura aniulie mwanangu.

 

                         Huku ni kumbipu au kumchezea sharubu Waziri Hamisi Kigwangallah (Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto) ambaye alishapiga marufuku huduma za afya kutolewa kwenye mazingira yanayohatarisha uhai wa mgonjwa badala ya kumponya.” Vifaa vyake vya maabara. Daktari huyo alinaswa wakati akiwa kazini akimfanyia vipimo dada mmoja na alipoulizwa alikiri kutoa huduma za matibabu kwa wakazi wa eneo hilo bila kuwa na kibali chochote katika duka lake hilo la dawa.

 

Kweli sina leseni, wala kibali chochote cha kuniruhusu kutoa huduma za matibabu hapa, lakini leseni ya duka la dawa ninayo, nipo kwenye process za kupata leseni ya kutoa huduma za vipimo hapa. “Nafanya hivi ili kujipatia riziki wanangu wale. Pia mke wangu ni mjamzito na huu ndiyo mwezi wake wa kujifungua, naombeni sana mnisamehe,” alijitetea jamaa huyo huku akichukuliwa picha mnato na video. Vifaa vya kazi.

 

MJUMBE SERIKALI YA MTAA Naye mjumbe wa serikali ya mtaa wa eneo hilo, Rashidi Bakari alikiri duka hilo kutoa huduma za kimatibabu bila kibali chochote. Hali ilivyokuwa. “Ni kweli anatoa huduma za matibabu hapa, lakini ni katika kuwasaidia wakazi wa hapa na maeneo mengine ya jirani,” alisema mjumbe huyo akiendelea kusisitiza kuwa ni kinyume na sheria. Hata hivyo, jamaa huyo aliishia mikononi mwa polisi ambao waliondoka naye kwenda kutoa maelezo kituoni ili hatua zaidi za kisheria zichukuliwe. Bango la kuingia kwenye pharmacy hiyo. Stori: Wandishi Wetu, Dar

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*