MSANII ABDU KIBA: SIJAMUONA WA KUSHINDANA NA SISI

        MSANII wa Bongo Fleva, Abdu Kiba, ameibuka na kuwatolea uvivu wale wote wanaosema kwamba kaka yake, Ally Kiba, amefulia kimuziki na kwa sasa hayupo kwenye soko la ushindani. “Tunachukulia ni changamoto kwa sababu sisi hatushindani, sisi tunafanya kazi, hatujamuona bado wa kushindana naye na hakuna mtu wa kushindana na sisi.

 

Ni mawazo tu ya mashabiki ambapo kila mtu ana uelewa wake na upendo wake. Kwenye kupendwa wakikutana wawili wanaweza kuanzisha ligi ambayo mimi huku nipo nakula zangu vizuri hata sijaona wa kushindana naye. Yaani kipindi wao wana-‘discuss’ , mimi bado sijaona wa kushindana naye ila tunachofanya tu ni muziki mzuri,” amesema Abdu Kiba.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*