MCHEKESHAJI ATADA NA BUSU LA MREMBO ELIZABETHI LULU

          Staa wa Bongo, Elizabeth Kimemeta Michael ‘Lulu’ akifanya yake na mchekeshaji kutoka nchini Kenya, Eric Moni stejini. Busu ‘makinikia’ alilomwagiwa na ‘mtoto mtamu’ kutoka Magufuli-land, Elizabeth Kimemeta Michael ‘Lulu’ limempa mawenge ya mwendokasi mchekeshaji kutoka nchini Kenya, Eric Mondi ambapo hakusita kuweka wazi hisia zake juu ya muigizaji huyo mwenye mvuto bomba.

 

View image on Twitter Twitter Ads info and privacy Akiwa jukwaani akitema madini yake ya vichekesho ndani ya Ukumbi wa King Solomoni jijini Dar siku ya Eid, Omondi alimtaja Lulu kama miongoni mwa wasanii wa kike Bongo wanaomvutia zaidi na bila kusita alimuita jukwaani kwa lengo la kupata japo wasaaa wa kupata busu lake, ombi ambalo Lulu alilitii na kilichofuata kinajieleza kwenye aya zinazofuata hapa chini. Mara baada ya

 

Lulu kupanda jukwaani, moja kwa moja alimfuata Eric na kumkumbatia kwa kumzungushia mikono kiuononi na kisha kumiminia mabusu mfululizo, hali iliyomchachawisha Eric na kupoteza ‘netiweki’ kwa muada, hali iliyoongeza shangwe miongoni mwa wahudhuriaji wengi. “Mtoto safi sana nyie acheni tu, ni miongoni mwa wasanii kutoka hapa TZ wananivutiaga sana, tazama mwenyewe anavyojiseti aiseeee,” alisikika Omondi akimsifia Lulu wakati muigizaji huyo akishuka jukwaani na kurejea kwenye sehemu yake ya kukaa

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*