KAJALA MASANJA AFUNGUKA HAYA KUHUSU MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA

                Staa wa filamu Bongo, Kajala Masanja amevunja ‘sefu’ ya kuhifadhia siri moyoni mwake na kuweka wazi kuwahi kujihusisha na ulevi wa madawa ya kulevya, aina ya bangi, Ijumaalina kauli yake. Katika mahojiano na mwandishi wetu hivi karibuni, msanii huyo alisema akiwa na umri wa kuingia usichanani kutoka utotoni, alijikuta mikononi mwa marafiki waovu, waliojihusisha na ulevi huo, ambao walifanikiwa kumteka akili na kumvutisha mmea huo, jambo ambalo anadai kulijutia kwa kiwango kisichotamkwa.

 

Kajala alisema licha ya kutumia bangi katika umri huo, hakudumu sana kwani aliachana nayo kufuatia jitihada kubwa za wazazi wake, huku akimshukuru Mungu kwamba hakuwahi kutopea kwenye madawa mengine ya kulevya. Msanii huyo mwenye figa bomba alitumia mwanya huo kuwaonya vijana kuchunga sana mzuka wa umri ambao huleta vishwishi vingi vya matamanio ya kidunia na kwamba ni vyema sana wazazi kuwa makini na watoto wanapofika katika umri wa balehe na kuvunja ungo, kwani ndicho kipindi kibaya maishani mwa binadamu na kuangalia sana aina ya watu wanaotengeneza nao urafiki.

 

Unajua inafika mahali sisi kama vioo vya jamii inatupasa kuzungumza ukweli wa maisha yetu husasan ya nyuma, ili kama ni watu kujifunza iwe hivyo, binafsi nimewahi kupitia maisha ambayo naweza kuyaita ya mpito, kipindi ambacho kila mtu hupitia katika harakati za ukuaji, kwamba nilijiingiza kwenye kampani za marafiki ambao ni watumiaji wa bangi.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*