JOYCE KIRIA AWAPA SOMO WAKAA UCHI MITANDAONI

                                   Mtangazaji wa Kipindi cha Wanawake Live, Joyce Kiria. KUTOKANA na matukio ya baadhi ya wanawake kujianika uchi mitandaoni kushika kasi, Mtangazaji wa Kipindi cha Wanawake Live, Joyce Kiria ameibuka na kuwapa somo kwamba, waachane na kujiuza, kisa njaa na kama wanapenda umodo, basi wafuate kanuni na taratibu za kimaadili na si kutumia njia hiyo.

 

                Staa wa Bongo, Gigy Money. Akizungumza na Risasi Jumamosi, Joyce alisema kuwa, anashangazwa na wanawake wanaojianika uchi mitandaoni hivyo kuwataka waache kwani baadaye watajutia baada ya kupata madhara makubwa. Amber Lulu “Mimi mwenyewe maisha ya kutegemea wanaume kwa kutafuta fedha nimeyaishi na yalinitesa sana maana unajikuta unajichosha na kujiingiza kwenye mambo ya hatari,” alisema Joyce.

         Joyce alimalizia kwa kusema kuwa, mwisho aliamua kutumia akili na hadi sasa ni mjasiriamali na fedha anayoipata anaifurahia kwani anaamini ni jasho lake.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*