Hii Kali!! Shilole kuolewa na mwendesha bodaboda kweli kila shetani na mbuyu wake

DAR ES SALAAM: Baada ya sarakasi nyingi za kubadili wanaume huku akizalishwa watoto wawili na kuingia katika kashfa ya kudaiwa kupenda kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanaume anaowazidi umri, hatimaye staa wa Muziki wa Bongo Fleva, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ amepata mwanaume wa kumuoa.

Chanzo makini kilicho karibu na staa huyo kilieleza kuwa kwa sasa amepata mchumba ambaye ni dereva wa bodaboda na wanatarajia kufunga ndoa ya siri kabla ya kuanza kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, akiwa amempata maeneo anayofanyia biashara yake ya chakula, Kinondoni Morocco, Dar.

“Shilole anatarajia kufunga ndoa na dereva bodaboda hivi karibuni kabla Waislamu kuingia kwenye Mfungo wa Ramadhan na itakuwa ya siri, nyie fuatilieni mtaujua tu ukweli,” kilisema chanzo.

Risasi Mchanganyiko lilifunga safari mpaka ofisini kwa Shilole, Kinondoni- Morocco ambapo alikiri kuwa na mchumba, lakini akikataa kumuweka wazi kwa sasa, lakini akikanusha kuwa siyo dereva wa bodaboda kama watu wanavyosema.

“Ni kweli nina mchumba, ila siyo dereva bodaboda, ni fundi magari, tuko kwenye utaratibu wa ndoa na nitawajulisha maana ndoa yangu haitakuwa ya siri, itakuwa ya wazi na itafungwa kwenye ndege,” alisema Shilole.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*