Hekaheka ya mpangaji achomwa kisu na mpangaji mwenzake wakigombea ndala

May 2, 2017 kupitia Heka heka ya Leo Tena ya Clouds FM mtangazaji Geah Habibu ametuletea hii stori iliyotokea Kiwalani ambako mpangaji mmoja kuchomwa kisu na mpangaji mwenzake kisa kikiwa ni ndala.

Inadaiwa kuwa mpangaji huyo alikuwa kwa masharti kwa wapangaji wenzake akiwaambia kuwa hataki mazoea na mtu na kuwaonya kuwa hata familia yake pia wasiizoee.

Kisa cha kumchoma kisu mpangaji mwenzake ni kwa sababu ya ndala za mpangaji mwingine kuvaliwa na mgeni wake hivyo kuzua vurugu zilizopelekea wawili hao kuzozana.

Bonyeza Play hapa chini kusikiliza full story.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*