HAJA KUBWA, Unajua unatakiwa kupata haja kubwa mara ngapi kwa siku? USIONE AIBU SOMA HAPA kama unatatizo litakwisha

Tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu ni jambo tunalolikwepa kwenye mazungumzo yetu ya kila siku. Hata hivyo ni tatizo kubwa katika jamii .

Kama kuna jambo unapaswa uliepuke kwa nguvu zote basi ni hili. Kwa afya bora kabisa hakikisha unapata choo kila siku mara 2 hata mara 3.

Kufunga kwa choo au kupata choo kigumu ndiyo chanzo kikubwa cha ugonjwa wa bwasiri kwa Tanzania, na hii inachangiwa kwa sehemu kubwa kwa kula ugali wa sembe na kutokunywa maji mengi kila siku.

Zifuatazo ni dawa 10 mbadala zinazotibu kufunga choo au choo kigumu:

1. Mafuta ya Zeituni

Mafuta ya zeituni (olive oil) yanatosha kutibu hili tatizo. Yana ladha nzuri mdomoni na ni dawa pia.Matumizi: Chukua kijiko kikubwa kimoja cha mafuta ya zeituni, changanya na kijiko kidogo kimoja cha chai cha maji maji ya limau na unywe asubuhi ukiamka tu tumbo likiwa bado tupu. Fanya hivi kila siku mpaka utakapopona.

Bottle pouring virgin olive oil in a bowl close up

2. Juisi ya Limauo

Juisi ya limau inatumika kutibu tatizo la kupata choo kigumu au kufunga choo. Chukua maji maji ya limau kutoka katika limau kubwa 3 na uchanganye na juisi ya matunda kupata kikombe kimoja (ml 250) na unywe yote kutwa mara 1 kila siku kwa siku kadhaa mpaka umepona.

3. Mazoezi ya kutembea

Kama unataka kupata choo kilaini na cha kawaida, basi jitahidi uwe mtu wa kutembea tembea na si kukaa tu kwenye kiti kutwa nzima.Jitahidi kila siku uwe unapata muda wa kutembea tembea kwa miguu mpaka dakika 60 au zaidi. Hii itakusaidia kuondoa tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu sana.

4. Vyakula vya nyuzi (fiber)

Mara nyingi utasikia watu wakisisitiza juu ya umuhimu wa kula vyakula vya asili na vyenye nyuzinyuzi. Chakula cha asili kina nafasi kubwa katika kuimarisha afya yako kwa ujumla.
Hakikisha pia asilimia 80 ya mlo wako kwa siku ni matunda na mboga za majani. Matunda kama ndizi na parachichi ni muhimu kula kila siku, kadhalika tumia unga au mbegu za maboga.

5. Aloe Vera

Ni muhimu utumie Aloe Vera fresh kwa kuchanganya vijiko vikubwa viwili vya jeli ya aloe vera ndani ya kikombe kimoja cha juisi ya matunda uliyotengeneza mwenyewe nyumbani (hasa juisi ya parachichi) na unywe yote kutwa mara 1 hasa nyakati za usiku unapokaribia kwenda kulala kwa siku kadhaa au mpaka umepona. Usitumie zaidi ya vijiko vikubwa viwili vya jeli ya Aloe Vera

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*