Baada ya askari kuuawa Kibiti, watu wawili wadakwa na fuvu la binadamu

Kibiti. Jeshi la Polisi mkoani Pwani linawashikilia watu wawili wakazi wa Kibiti kwa tuhuma za kukutwa na fuvu la kichwa cha binadamu.

Akithibithisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Pwani, Onesmo Lyanga amesema watu hao walikamatwa mwishoni mwa wiki iliyopita wakati polisi wakiwa kwenye doria katika kijiji ya Jaribu.

Lyanga amesema watuhumiwa hao waliokuwa wakitoka Mkuranga kuelekea Kibiti kwa kwa kutumia pikipiki walikuwa wameficha fuvu hilo kwenye begi.

Amesema baada ya kufika katika kijiji hicho wakiwa kwenye pikipiki walisimamishwa na polisi waliokuwa doria eneo hilo na baada kuwakagua ndipo walipokuta fuvu hilo ndani ya begi.

Amesema uchunguzi unaendelea ili kubaini mahali lilipotoka fuvu hilo.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*